Deuteronomy 25:17-19

17 aKumbuka kile Waamaleki walichowatendea mlipokuwa njiani mkitoka Misri. 18 bWakati mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu. 19 cBwana Mungu wako atakapokupa pumziko mbali na adui zako wote wanaokuzunguka katika nchi akupayo kuimiliki kuwa urithi, utafutilia mbali kumbukumbu lote la Waamaleki chini ya mbingu. Usisahau!

Copyright information for SwhNEN